James Kotei anaweza kujiunga na Zesco United ya Zambia endapo Zesco wataweza kufika makubaliano binafsi na Kotei pamoja na Klabu yake Kaizer Chiefs ambayo inataka kumtoa kwa mkopo wa miezi 6,
Awali Kotei alikuwa anahusishwa kujiunga na Klabu Yanga kwa mkopo, inaelezwa kuwa vilabu vya Yanga na Kaizer vilishafika makubaliano ya kiungo huyo kijiunga na Yanga lakini Kotei amekataa na kueleza kuwa ikiwa anahitaji kurudi Tanzania basi Klabu atakayojiu nga nayo ni klabu ya Simba tu kutokana heshima aliyoipata wakati anaichezea Klabu hiyo ya Simba.

-Kwa ufupi sakata la James Kotei
Inavyoonekana ni Kama Kaizer wanamlazimisha kumpeleka James kotei Yanga lakini Kotei hayupo tayari na hiyo imekuja baada ya dili la Kaizer chief kumpeleka Kotei Simba kugonga mwamba.
Baada ya James Kotei kukosa nafasi katika kikosi cha Kaizer Chief waliamua kutafuta mbadala wake, na chaguo lao la kwanza lilikuwa ni kiungo wa kimataifa wa Kenya anayechezea klabu ya Zesco united Anthony Akumu na waliweka wazi kabisa kwamba watampeleka James Kotei kwa mkopo katika Klabu ya Simba lakini klabu ya Simba hawakuonyesha nia kumuhitaji Kotei kwasababu tayari wana viungo wengi
Yanga kupitia wadhamini wao wa GSM Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Injinia Hersi Said alipoalikwa kuhudhuria hafla ya maadhimisho ya miaka 50 klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini alitumia fursa hiyo kufungua ukurasa wa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya soka na kwa kuanza klabu ya Kaizer chief ikataka kumpeleka James kotei kwa mkopo katika Klabu ya Yanga lakini bahati mbaya Kotei ameweka ngumu kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania bara sababu kubwa ikiwa ni heshima aliyoipata Simba.
-Kaizer Chiefs wanalazimisha Kotei aende Yanga, Kotei amegoma Tusubiri tuone mwisho wa hii vita.
