-Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Luc Aymeal ameshaanza kazi ndani ya Klabu ya Klabu ya Yanga. Klabu hiyo inajiandaa na michezo minne (4) ndani ya mwenzi huu itacheza michezo 3 za ligi kuu Tanzania Bara na mmoja wa Kombe la Azam Sports federation Cup.

-Keshokutwa ya January 15 itacheza dhidi ya Kagera Sugar, January 18 dhidi ya Azam FC, January 25 itacheza mchezo wa ASFC dhidi ya Tanzania Prisons, January 30 itacheza dhidi ya Biashara United. Michezo yote minne (4) itachezwa jijini Dar.

-Klabu ya Bandari FC ya Kenya, imemfuta kazi kocha mkuu wa klabu hiyo Benard Mwalala kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi kuu soka nchini Kenya. Bandari FC mpaka sasa imecheza michezo 16 za ligi na kufanikiwa kukusanaya pointi 18 tu. Klabu hiyo imemtangaza kocha, Twahir Muhiddin kuwa kocha wa muda hadi kocha mpya atakapotangazwa.