-Klabu ya Real Madrid wamefanikiwa kutwaa Kombe la Spanish Super Cup baada ya kuibuka na ushindi Penati 4-1 dhidi ya Atletico Madrid baada ya dakika 120 kuisha kwa bila kufungana (0-0).

-Kiungo wa Real Madrid Federico Valverde alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo wa Fainali ya Super Copa ya Hispania Kati ya Real Madrid dhidi ya Atletical Madrid. Pamoja na kushinda tuzo hiyo Valverde hakumaliza mchezo huo baada ya dakika 115 kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Morata ambaye alikuwa anaenda kufunga.