-Aliyekuwa Kaimu kocha mkuu wa Klabu ya Yanga, Boniface Charles Mkwasa anatarajia kutangazwa kuwa mkurungezi wa Ufundi ndani ya Klabu ya Yanga hiyo umekuja baada ya kocha mkuu wa Klabu Luc Eymael kuomba kupewa kocha msaidizi mwingine tofauti na Mkwasa. Kwa mujibu wa habari kutoka Yanga zinadai kuwa Ijumaa ya January 17 Yanga itamtangaza Kali Ongala kuwa kocha msaidizi.

-Klabu ya Polisi Tanzania imekamilisha Usajili wa golikipa Peter Manyika Jr kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Klabu ya KCB ya Kenya.

-Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe, Never Tigere kutoka Klabu ya Platinum inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini kwa mkataba wa mwaka mmoja.
