Kikosi cha mabingwa wa Tanzania Bara Klabu ya Simba tayari wamewasili jijini Mwanza wakitokea visiwani Zanzibar, Simba itacheza dhidi ya Mbao FC siku ya Alhamisi katika dimba la Kirumba , mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuvaana na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu Tanzania barani kesho Jumatano saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Uhuru.