Shirikisho la soka nchini Lesotho limempiga faini mchezaji wa klabu ya Lesotho Defense Force FC (LDF FC) ya M10,000 sawa na ($695) na kuwafungia wachezaji wengine watano wa klabu hiyo kutocheza mechi tatu zijazo za Ligi Kuu.
Hayo yalitokea baada ya wachezaji hao kutoka nje ya uwanja wakati mechi ikiendelea ambayo ilikuwa nusu fainali ya mashindano ya Independence Cup 2019 dhidi ya Matlama FC baada ya mwamuzi kuwapa Matlama bao nililokuwa na utata kipindi cha pili cha mchezo huo.

-Shirikisho la Soka nchini Misri (EFA) limeanzisha mafunzo kwa waamuzi juu ya matumizi ya teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR), inayotarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.
