-Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Meddie Kagere Leo atakosekana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC Kutokana na kuwa na kadi Tatu za njano.
-Klabu ya Yanga kwenye dirisha dogo la Usajili lilofungwa Jana usiku imefanikiwa kusajili Wachezaji 6 wapya huku ikiwawacha wachezaji 6 wa kimataifa na kuwatoa Wachezaji 4 kwa mkopo. Wachezaji waliosajiliwa ni Adeyun Saleh, Tariq Seif, Ditram Nchimbi, Kiungo Fundi Haruna Nyonzima, Mshambuliaji Ykpe Gnamien na Winga Bernad Marrison.
-Wachezaji waliondoka Yanga walioachwa kwa kuvunjiwa mikataba ni Sadney Urikobh, Juma Balinya, Issa Bigirimana, Maybin Kalengo, Mustapha Seleiman na Mshambuliaji David Molinga Falcao waliotolewa kwa mkopo ni Saad Kassim na Said Mussa Bakari wote Lipuli FC, Cleofas Sospeter na Mwarami Isaa wote Singida United. Pia Yanga imeleta bechi jipya la Ufundi likiongozwa na kocha Luc Eymael.

-Klabu ya Simba Katika dirisha dogo lilofungwa Jana usiku imefanikiwa kusajili wachezaji wawili na kukuacha mchezaji mmoja. Waliosajiliwa ni mawinga Luis José Miquissone Raia wa Msumbiji na Ramadhani Shiza Kichuya huku ikitangaza kuachana na Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Wilker Henrique Da Silva.

-Klabu ya Azam FC Katika dirisha dogo lilofungwa Jana usiku imefanikiwa kusajili wachezaji wawili na kumuacha mchezaji mmoja waliosajiliwa na Azam Ni Khleffin Hamdoun wa Zanzibar na kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe Never Tigere huku ikiachana na Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Seleman Ndikumana.

