-Kocha mpya wa Yanga, Luc Eymael amewakataza wachezaji wa Klabu ya Yanga kutotumia usafiri wa pikipiki (Bodaboda) kwa lengo la kuwahi mazoezi yake. Eymael amesema wachezaji wote wanatakiwa kutumia basi la klabu hiyo wakati wa kwenda mazoezini.
-Kocha huyo alisema wachezaji wanapokuwa hawapo kambini watakiwa kufika klabuni mapema ili waweze kuondoka kwa pamoja, lakini si kupanda pikipiki. “Usafiri wa basi la klabu ni salama zaidi kuliko kutumia usafiri wa pikipiki pia itasaidia wote kufika kwa wakati mazoezini,” alisema Eymael.
Klabu ya AS Vita Club ya DR Congo imemuuza beki wao, Moustapha Luete Ava Dongo kwenda katika Klabu ya Ligi Kuu nchini Ubelgiji,Royal Antwerp Amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu kwa dau la Uhamisho wa €350,000 kuitumikia Klabu hiyo. Luete 23; Alijiunga na Vita msimu huu akitokea Jeunesse Sportive ya hapo hapo DR Congo.

