-Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu mkuu wa Klabu hiyo Dr David Luhago umeilalamikia Bodi ya ligi (TPLB) kwa kubadilisha sehemu ya mchezo wao dhidi ya Singida United kutoka Arusha kurudi Singida huku wao wakiwa wameshafanya maandalizi ya awali Arusha.

-Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Luhago amesema tayari wameshafanya maandalizi ya usafiri kwa kuweka booking kwenye ndege na kulipa sehemu ya pesa (advance) kwenye hoteli watakayo fikia hivyo hawaelewi jinsi ya kurudisha gharama zao baada ya mabadiliko hayo.

-Dk. Luhago amesema kwa kawaida kama kuna mabadiliko ya ratiba ya mchezo taarifa inapaswa kutolewa saa 48 kabla lakini Bodi haikufanya hivyo na kuwashtukiza kuwaambia mchezo huo utapigwa mkoani Singida sio Arusha tena. Mchezo huo utachezwa Jumanne ya January 21.

-Naomba msamaha kwa wana mchezo wote kwa kadi niliyoipata siku ya jana na tukio nililofanya kwenye mchezo wetu vs Azam fc,kweli mchezo wa mpira ni mchezo wa furaha na upendo kwa kuwa ni ajira ila changamoto za hapa na pale zipo,pia naomba msamaha kwa wachezaji, viongoz wangu wa Yanga SC na pia hata wa Azam FC na hata viongozi wenye dhamana na soka letu Tanzania Football na sitaweza kuja rudia tukio la aina ile.