Habari njema kwa Watanzania na wapenda soka kwa ujumla ni kwamba zile tetesi na Joto joto la usajili wa Samatta zimetimia rasmi, ambapo Mbwana Samatta amesaini Kandarasi Baabu kubwa la Miaka Minne na Miezi Sita! Ndani ya Klabu ya Aston Villa FC.

-Na kubwa ZAIDI la pili ni kwamba Lugha adhimu kabisa ya Kiswahili yazidi kuwa tamu na kupaa ZAIDI duniani ambapo Leo Samatta amekaribishwa na Klabu yake mpya ya Aston Villa FC kwa maneno ya Kiswahili Fasaha ”KaribuSamatta”