Meneja wa Aston Villa Dean Smith amesema mkataba wa kumsajili Mbwana Samatta ‘uko karibu sana’ kukamilika, lakini amethibitisha kuwa hatoweza kucheza mechi ya kesho dhidi ya Watford.

Smith amesema kilichosalia sasa ni mambo madogo madogo sana na “hakuna wasiwasi wowote” katika uhamisho huu.

Samatta anaweza hata kutangazwa hii leo lakini hatoweza kucheza mechi ya kesho kwa sababu wachezaji lazima waandikishwe kabla ya saa za mchana siku moja kabla ya mechi.

Dean amesema “Tungependa awepo kwenye mchezo wa Watford, lakini hata kama ingekuwa hivyo angekuwa na muda mfupi sana [wa maandalaizi] na wachezaji wenzake.”