-Uongozi wa klabu ya Lipuli FC ya Mkoani Iringa umeliandikia barua Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumshtaki aliyekuwa kocha wake Haruna Harerimana Raia wa Burundi kwa kuacha kuifundisha timu hiyo kinyume na mkataba waliojiwekea.

-Kaimu mwenyekiti wa Lipuli, Ayubu Kihwelo amesema kuwa tayari wamemuandikia barua kocha huyo na TFF kutokana na kocha huyo kuonekana katika benchi ya ufundi la KMC kinyume na utaratibu. Pia kusaini mkataba na KMC akiwa na mkataba halali na Lipuli ambao ulikuwa unaisha July mwaka huu.

-Mshambuliaji kinda wa Uganda, Allan Okello mwenye umri wa miaka 19 amejiunga rasmi na klabu ya Paradou ya Algeria akitokea KCCA ya Uganda kwa dau la dola 200,000 (zaidi ya milioni 460 za Kitanzania).